Search This Blog

Friday, March 18, 2016

KLABU BINGWA ULAYA DROO KUFANYIKA LEO IJUMAA


Klabu 8 toka Nchi 5 Leo Ijumaa zitatumbukizwa
kwenye Chungu kimoja kwenye Droo ya kupanga
Mechi za Robo Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONS
LIGI, kwenye shughuli itakayofanyika huko Nyon,
Uswisi.
Droo hii iko wazi ikimaanisha Timu za Nchi moja
zinaweza kukutanishwa na hivyo upo uwezekano
wa, mathalani, Real Madrid na Barcelona kukutana.
Klabu zilizofuzu kuingia Robo Fainali:
-Atlético Madrid
-Bayern München
-Barcelona
-Benfica
-Manchester City
-Paris Saint-Germain
-Real Madrid
-Wolfsburg