Search This Blog

Saturday, March 12, 2016

EUROPA LEAGUE MANCHESTER UNITED YAAMBULIA KIPIGO

Hatua ya 16 bora ya michuano ya Europa
League ilianza usiku wa jana kwa timu zote
16 kujitupa viwanjani kusaka ushindi wake wa
kwanza katika mechi mbili za hatua hii.
Manchester United wakisafiri ugenini kuwavaa
Liverpool katika dimba la Anfield na wenyeji
Liverpool waliibuka na ushindi wa bao 2-0
katika mchezo ambao uliotawaliwa na Liverpool
huku United wakipoteana hasa Kipindi cha
kwanza hali iliyopelekea wasiweze kupata
hata shuti moja lililolenga lango kwa kipindi
hicho cha kwanza.
Liverpool walipata magoli yao kupitia kwa
Daniel Sturadge kwa njia ya penati na Roberto
Firminho aliyetumia uzembe wa Michael Carrick
ambaye aliingia kucheza beki wa kati
akichukua nafasi ya Rashford.