Search This Blog

Saturday, March 19, 2016

DIAMOND AMKUMBUSHA RAIS MAGUFULI

Msanii mahiri nchini anaeipeperusha vyema
bendera ya Tanzania nje ya nchi Nassib Abdul
maarufu kama Diamond Plutnumz, amemkumbusha
Rais Magufuli kuhusu ahadi yake ya kushughulikia
kujenga ukumbi wenye hadhi ya kimataifa ambao
utaweza kuruhusu kufanyika shughuli mbalimbali za
kimuziki.
Akizungumza na kipindi cha XXL kinachorushwa na
Clouds FM Diamond Plutnumz amesema aliwahi
kupiga story na rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Magufuli na kumuomba kupitia
serikali yake aweze kuwajengea ukumbi mkubwa
wasanii utakao wasaidia kupanua wigo wa muziki
nchini kwa shughuli za kimataifa kama tuzo kubwa
kufanyikia nchini.
Diamond amezidi kueleza kuwa amewahi
kuambiwa na baadhi ya waandaaji wa tuzo kuwa
wanampango wa kuja kufanyia tuzo nchini
Tanzania lakini tatizo hakuna ukumbi mkubwa wa
kumudu tukio hilo la aina yake, hivyo Diamond
amemuomba Rais Magufuli asiwasahau atimize
ahadi yake, ili tasnia ya muziki izidi kusonga mbele.